Asilimia kubwa sana ya watu wanataka kuwa matajiri na inawezekana kwasababu unakuta mtu ana mtaji mkubwa,mipango ya biashara yake lakini anakwama kwasababu ya tabia hizi zifuatazo
01.Acha kuahirisha mambo
Hii unamkuta mtu kila kukicha anasema kesho ntaanza kufanya kitu fulani kesho inapofika anapeleka mbele tena tarehe ya kufanya kitu cha mafanikio.kama unataka kuwa tajiri achana na tabia hiyo kabisa kikubwa heshimu muda
02.Acha tabia ya kuweka wazi mipango yako ya maendeleo
Watu wengi huwa wepesi kuweka mipango yao wazi kwa malengo tofautitofauti aidha kuwaonyesha watu mipango yako ili wakupe heshima .lakini kaa ukijua sio watu wote wanapenda maendeleo yako kwahiyo kukufanyia vitu vibaya au kuiga malengo yako ni rahisi sana
03.Acha tabia ya kutojiwekea akiba
pia hili ni tatizo wengi wetu sana lakini tunatakiwa kuacha kwasababu kuweka akiba kuna saidia sana siku kama umekwam katika biashara kuchukua kiasi katika akiba yako na kuendelea kusonga mbele kimafanikio
04.Acha kutumia vibaya pesa
hili watu wengi sana tunalo lakini tunatakiwa kutambua kuwa tunavotumia vibaya pesa kuendelea kimafanikio ni vigumu sana kwasababu pesa hizo tunazozitumia vibaya tungeweza kuzitumia katika biashara na kufikia mafanikio makubwa
IMEANDIKWA NA YUSUPH SWALEH
ENDELEA KUTUFUATIA PIA YOUTUBE KWA KUANDIKA YUZHASSAL TV
0 comments :
Chapisha Maoni