FOR THE ENTERTAINMENT UPDATES & INTERVIEWS

Jumamosi, 25 Novemba 2017

TIBA ASILI YA M'BA KATIKA NYWELE HII HAPA

JINSI YA KUONDOA MBA KWENYE NYWELE ZAKO KWA KUTUMIA LIMAO AU NDIMU!

Wengi tunasumbuliwa sana na mba katika nywele zetu.
Je Unajua njia za Kuondoa tatizo la mba katika nywele?
Kuna njia nyingi za asili za kuondoa mba kwenye nywele , Leo tutaangalia moja Kati ya njia hizo; lakini kwanza tuangalie, je mba zinasababishwa na nini?

Hili ni swali ambalo mara nyingi wengi wetu tunawezatoa majibu tofauti kwa kudhani Mba zinasababishwa na uchafu pekee katika nywele.
Lakini ukweli ni kwamba mba zinasababishwa pia na ukavu wa ngozi inayobeba nywele zako.

JINSI YA KUONDOA MBA KWA KUTUMIA LIMAO AU NDIMU!

Limao na ndimu ni matunda unayoweza kutumia kuondoa mba katika nywele zako.
Kuna njia mbili za kutumia LIMAO AU NDIMU

Njia ya kwanza ni kata limao katika vipande, kamua maji yake kama kijiko kimoja hivi kisha jaribu kupaka hayo maji katika ngozi ya kichwa chako bila kuchanganya na vitu vingine. Hapa paka hayo maji ya limao chini ya ngozi na kwenye nywele. Baada ya dakika kadhaa osha nywele zako kwa maji safi.

Njia ya pili ya limao ni, kamua maji ya limao kijiko kimoja changanya na maji safi ambayo hayajachanganywa na kitu chochote, kisha osha nywele zako.
Fanya hivyo kila unapohitaji kuosha nywele kwakutumia mchanganyiko huo kama shampuu.

Faida za Limao au Ndimu katika Nywele!
Matunda haya yana citric acid ambayo pia husaidia kuondoa fangasi katika nywele.

Pia ni tiba kwa magonjwa ya ngozi kwa ujumla katika mywele. 
Vilevile limao na ndimu husaidia nywele zikue haraka.


Maoni 2 :

  1. Mmba hawa ktk nywele wanasumbua wenye utaalam na wadudu hawa endeleeni kutujuza kadri ya uwezo na utafiti wenu asnteni

    JibuFuta
  2. Asante kwa tiba yako ya maelezo tutajarbu kufanya hivyo

    JibuFuta