kwa kuanza kabisa habari ndugu wafatiliaji wa yuzhassal tv blog
najua watu wengi wanafikiria na wanahisi ni bora kujiajiri kuliko kuajiriwa hiyo ni sawa lakini wengi hukurupuka kuanza kujiajiri jambo ambalo mda mwingi linaleta madhara makubwa na mtu kuanza kujutia kwanini kaacha kazi alipokuwa ameajiriwa na kujiajiri mwenyewe
jambo hilo la kukurupuka kujiajiri ni baya sana kikubwa fahamu ata huyo boss wako kajiajiri ndipo akakuajiri wewe ukishagundua hilo tuliza akili pangilia mipango yako ya jinsi gani utaendesha biashara yako kwa kujiajiri wewe mwenyewe
HAYA NDIO MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUJIAJIRI
01. JENGA HESHIMA; najua wengi mtakuwa mnajiuliza nijengaje heshima hii ipo hivi unatakiwa uheshimu kwanza kile ambacho unachotaka kukifanya baada ya hapo heshimu muda wako .kama hauwezi kuuheshimu ata mda wako wa kazi daima utajutia tu kujiajiri kwasababu unapojiajiri amna mtu wa kukupelekesha kwamba mda huu fanya kitu fulani hapo ni wewe mwenyewe
kwahiyo tunatakiwa kuheshimu muda wetu
02. TAMBUA JAMII INATAKA NINI KWA WAKATI HUO;hili ni jambo kubwa sanaunapotaka kujiajiri hakikisha jamii inayokuzunguka inataka nini kwa mda huo
yaani kwa upande mwingine changamoto ambayo ipo kwa wakati huo katika jamii yako hiyo ndio fursa kwako kuanzisha biashara ambayo itakuingizia pesa nyingi sana
03.JIUNGE NA WAJASIRIAMALI/WAFANYA BIASHARA WALIOKUTANGULIA;
pia hichi ni kitu kitakachokusaidia sana wewe unayetaka kujiajiri kama wote tunavojua kuwa kila biashara ina changamoto zake kwahiyo unapojichanganya na wajasiriamali/wafanya biashara waliokutangulia utafahamu changamoto utakazoenda kukutana nazo mbele lakini hiyo haitakuwa mbaya kwako kwasababu tayaari umepewa njia ambazo utazitumia kupambana na changamoto hizo kwa kujichanganya na wajasiliamali/wafanyabiashara
04. BIDII;kama wote tunavojua kuwa katika kujiajiri kunahitaji bidii sana kwasababu tuchukulie mfano kwamba wapo wafanyabiashara wa nguo watano katika eneo moja nawewe upo ndani ya hao
swali unaweza kufanikiwa pasipo kuongeza bidii kwa kupunguza nguo bei kidogo ili kuweza kuwavutia wateja kikubwa bidii bidii bidii
05.FURAHIA UNACHOKIFANYA;siku zote ukifurahia unachokifanya utafanya kitu bora kwasababu utafanya kwa moyo mmoja .kwahiyo wewe unayetaka kujiajiri na biashara uliyoichagua haufurahii kuifanya nakushauri ACHA BIASHARA HIYO kwasababu huko ni kupoteza muda na pesa zako mafanikio hutayapata kamwe kwasababu hutoifanya kwa mikono miwili
06.TAFUTA ENEO ZURI LA KUFANYIA BIASHARA;Hili ni la muhimu sana kwa sababu ukitafuta eneo zuri ambalo mfano kuna mkusanyiko wa watu lazima upate pesa kwasababu ya mkusanyiko huo wa watu
MUHIMU: utakapowekeza pesa nyingi ndipo utapata pesa nyingi zaidi pia ukafata mambo hayo kufanikiwa lazima
kama una maoni ushauri tuachie apo chini ili kwa umoja wetu tuyafikie mafanikio
IMEANDIKWA NA YUSUPH SWALEH
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
0 comments :
Chapisha Maoni