JE UNAFAHAMU KUNA BAADHI YA VITU UKIVIFANYA BAADA YA KULA UNAJISABABISHIA MATATIZO MAKUBWA
Hiyo ni kweli kuna baadhi ya vitu ukivifanya muda mfupi baada ya kula unajisababishia matatizo makubwa baadhi ya vitu hivyo ni;
kuoga Hii ni kwasababu ifuatayo baada ya kula chakula bila ya kupumzika angalau dakika 30
ukienda kuoga utasababisha mmeng'enyo wa chakula kufanyika haraka sana tofauti na hali ya kawaida kwasababu katika kitendo cha kuoga watu wengi hutumia nguvu nyingi katika kusugua miili yao hali inayopelekea mmeng'enyo kufanyika haraka
kula matunda Hii najua watu wengi mtashangaa lakini ndivyo ilivyo kuwa ukila matunda pale tu ulipomaliza kula chakula uko hatarini kupata matatizo makubwa sana kwasababu mmeng'enyo wa matunda huchukua mda sana kuliko wa chakula cha kawaida
hivyo unashauriwa kula matunda angalau nusu saa au lisaa kabla ya kula chakula ili pindi ambapo utakula chakula mimeng'enyo yote ya chakula na matunda iweze kwenda sawa
kutembea au kukimbia Pia hii ni hatari kubwa sana kwasababu unatakiwa kupumzika angalau nusu saa baada ya kula lakini pindi unavyokula tu na kuanza kukimbia au kufanya mazoezi kwa ujumla hiyo itasababisha mmeng'enyo wa chakula kufanyika haraka sana jambo ambalo halifaii
kulala Hii ni kwa wale wanaokula nakulala papo kwa papo
kitaalamu tunaambiwa ni vema sana kama tukipata chakula tunatakiwa kupumzika angalau nusu saa au lisaa kabisa kabla ya kulala jambo hilo la kupumzika litasaidia mmeng'enyo wa chakula kufanya kazi vizuri na kukuwezesha kuwa na afya njema
lakini pindi utakapokula chakula tu na kulala mmeng'enyo wa chakula hautafanya kazi jambo linalosababisha matatizo makubwa sana katika miili yetu
ahsante kwa kuwa na mimi katika elimination iyo endelea kuifatilia blog yetu (yuzhassal.blogspot.com)
0 comments :
Chapisha Maoni