Hapo mwanzoni kulikuwa na habari kwamba kocha Jose Mourinho angeongeza mkataba mpya utakaomuweka OT hadi mwaka 2022, lakini habari imebadilika na habari ni Jose Mourinho kuondoka United.
Mourinho ambaye amekuwa hana tabia ya kudumu katika klabu moja amesema ana uhakika hatamaliza kazi yake ya ukocha katika klabu hiyo na baada ya muda atakwenda kwingine, wapi anaweza kwenda hapo baadae?
Bayern Munich, kocha wa sasa wa Munich Jupp Heynckes mkataba wake na timu hiyo unaishi mwisho wa msimu huu, Mourinho anependa siku moja kupata mafanikio Ujerumani na hata kama sio msimu ujao inawezekana siku moja mbeleni Mou akatua Bayern Munich, mapenzi yake na vilabu vikubwa pia inaweza kumvuta Bayern.
Paris Saint German, amepata mafanikio Hispania, Italia, Uingereza na ni wazi angependa kwenda katika ligi nyingine yenye mvuto na inayokuja kwa kasi ulimwenguni, PSG ni mahala sahihi kwa Mourinho na patakuza sana jina la klabu.
Uingereza, kuna wakati nchini Uingereza Jose Mourinho alikuwa akipigiwa chapuo kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, japo hilo bado halijatokea lakini ni wazi baada ya mafanikio katika klabu Mou angependa kupata mafanikio timu ya taifa.
Ureno, ukiachana na Waingereza kumtaka lakini yeye Jose Mourinho amewahi kukiri kwamba kabla hajastaafu angependa kuifundisha nchi yake, kwa umri alionao hivi sasa inawezekana ndio muda sahihi wa kurudi nchini kwao kujiunga na timu ya taifa ya Ureno.
China League, Wachina nao huwezi kuwaacha kila mahala unapozungumzia jina kubwa, wanatumia nguvu kubwa ya pesa kujaribu kushawishi majina makubwa kuhamia katika vilabu vyao, na kama walivyowashawishi kina Carlos Tevez wanaweza kumshawishi pia Jose MourinhO
0 comments :
Chapisha Maoni