FOR THE ENTERTAINMENT UPDATES & INTERVIEWS

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo News. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo News. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 1 Januari 2018

MASOUD KIPANYA AIBUKA

Baada ya habari kuenea kila kona ya Tanzania na nje ya nchi pia hatimaye mtangazaji wa power breakfast ya clouds FM na mchora katuni masoud kipanya ameweza kuibuka instagram na kupost ujumbe kama unavouona katika picha hiyo
Kwa mbivu na mbichi ili kujua ni kipi kilichomsibu usikose kutizama kesho asubuhi clouds 360 ndani ya clouds tv
Imeandikwa na yusuph swaleh

Jumamosi, 25 Novemba 2017

TIBA ASILI YA M'BA KATIKA NYWELE HII HAPA

JINSI YA KUONDOA MBA KWENYE NYWELE ZAKO KWA KUTUMIA LIMAO AU NDIMU!

Wengi tunasumbuliwa sana na mba katika nywele zetu.
Je Unajua njia za Kuondoa tatizo la mba katika nywele?
Kuna njia nyingi za asili za kuondoa mba kwenye nywele , Leo tutaangalia moja Kati ya njia hizo; lakini kwanza tuangalie, je mba zinasababishwa na nini?

Hili ni swali ambalo mara nyingi wengi wetu tunawezatoa majibu tofauti kwa kudhani Mba zinasababishwa na uchafu pekee katika nywele.
Lakini ukweli ni kwamba mba zinasababishwa pia na ukavu wa ngozi inayobeba nywele zako.

JINSI YA KUONDOA MBA KWA KUTUMIA LIMAO AU NDIMU!

Limao na ndimu ni matunda unayoweza kutumia kuondoa mba katika nywele zako.
Kuna njia mbili za kutumia LIMAO AU NDIMU

Njia ya kwanza ni kata limao katika vipande, kamua maji yake kama kijiko kimoja hivi kisha jaribu kupaka hayo maji katika ngozi ya kichwa chako bila kuchanganya na vitu vingine. Hapa paka hayo maji ya limao chini ya ngozi na kwenye nywele. Baada ya dakika kadhaa osha nywele zako kwa maji safi.

Njia ya pili ya limao ni, kamua maji ya limao kijiko kimoja changanya na maji safi ambayo hayajachanganywa na kitu chochote, kisha osha nywele zako.
Fanya hivyo kila unapohitaji kuosha nywele kwakutumia mchanganyiko huo kama shampuu.

Faida za Limao au Ndimu katika Nywele!
Matunda haya yana citric acid ambayo pia husaidia kuondoa fangasi katika nywele.

Pia ni tiba kwa magonjwa ya ngozi kwa ujumla katika mywele. 
Vilevile limao na ndimu husaidia nywele zikue haraka.


Jumamosi, 21 Oktoba 2017

UKITAKA KUWA TAJIRI ACHA TABIA HIZI

Asilimia kubwa sana ya watu wanataka kuwa matajiri na inawezekana kwasababu unakuta mtu ana mtaji mkubwa,mipango ya biashara yake lakini anakwama kwasababu ya tabia hizi zifuatazo
01.Acha kuahirisha mambo
Hii unamkuta mtu kila kukicha anasema kesho ntaanza kufanya kitu fulani kesho inapofika anapeleka mbele tena tarehe ya kufanya kitu cha mafanikio.kama unataka kuwa tajiri achana na tabia hiyo kabisa kikubwa heshimu muda
02.Acha tabia ya kuweka wazi mipango yako ya maendeleo
Watu wengi huwa wepesi kuweka mipango yao wazi kwa malengo tofautitofauti aidha kuwaonyesha watu mipango yako ili wakupe heshima .lakini kaa ukijua sio watu wote wanapenda maendeleo yako kwahiyo kukufanyia vitu vibaya au kuiga malengo yako ni rahisi sana 
03.Acha tabia ya kutojiwekea akiba
pia hili ni tatizo wengi wetu sana lakini tunatakiwa kuacha kwasababu kuweka akiba kuna saidia sana siku kama umekwam katika biashara kuchukua kiasi katika akiba yako na kuendelea kusonga mbele kimafanikio
04.Acha kutumia vibaya pesa
hili watu wengi sana tunalo lakini tunatakiwa kutambua kuwa tunavotumia vibaya pesa kuendelea kimafanikio ni vigumu sana kwasababu pesa hizo tunazozitumia vibaya tungeweza kuzitumia katika biashara na kufikia mafanikio makubwa
IMEANDIKWA NA  YUSUPH SWALEH
ENDELEA KUTUFUATIA PIA YOUTUBE KWA KUANDIKA YUZHASSAL TV

Ijumaa, 20 Oktoba 2017

HIVI NDIVO KESI YA SCORPION INAVYOENDELEA

Mahakama ya Wilaya ya Ilala Oktoba 31,2017 itatoa uamuzi iwapo mshtakiwa Salum Njwete maarufu Scorpion ana kesi ya kujibu au la.

Uamuzi utatolewa baada ya leo Ijumaa Oktoba 20,2017 upande wa Jamhuri kufunga ushahidi katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho, Said Mrisho inayomkabili Njwete (34).

Katika hati ya mashtaka, Njwete anayewakilishwa na wakili Juma Nassoro anadaiwa kutenda makosa hayo Septemba 6,2016 saa nne usiku eneo la Buguruni wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka, Salum Masoud mkazi wa Buguruni ambaye ni mfanyabiashara wa kuuza chenji katika kituo cha daladala amedai siku ya tukio alikuwa katika biashara zake.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule alidai akiwa katika shughuli zake alishuhudia mabishano kati ya mshtakiwa na mteja aliyekuwa akinunua bidhaa eneo hilo.

Amedai alimuona mshtakiwa akigonga meza akimlazimisha mteja huyo kumfuata.

Shahidi huyo alidai mteja huyo alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu hivyo alikataa kwenda.

Masoud alidai alimuona mshtakiwa akimfuata mteja huyo, kumvuta, kumwangusha chini na kuanza kumpiga maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Amedai alimwona mshtakiwa akichomoa kisu na kumtoboa mteja huyo na alisikia sauti ya kilio chake cha kuomba msaada, huku akitokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Shahidi huyo alidai mshtakiwa alichukua mkufu aliokuwa amevaa mteja huyo shingoni na uliokuwa mkononi. Pia, alidai alichukua pochi iliyokuwa mfukoni na alimsukuma kwenye Barabara ya Mandela ambako alianguka.

Baada ya mshtakiwa kuondoka, Masoud anadai walimnyanyua mteja huyo na kumweka eneo la wazi linalotenganisha barabara.

Amedai mtu aliyekuwa eneo hilo alitoa taarifa polisi ambao walifika eneo hilo na kuwatawanya kabla ya kumchukua majeruhi na kumpeleka hospitali.
KUTOKA MUUNGWANA

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUJIAJIRI

kwa kuanza kabisa habari ndugu wafatiliaji wa yuzhassal tv blog 
najua watu wengi wanafikiria na wanahisi ni bora kujiajiri kuliko kuajiriwa hiyo ni sawa lakini wengi hukurupuka kuanza kujiajiri jambo ambalo mda mwingi linaleta madhara makubwa na mtu kuanza kujutia kwanini kaacha kazi alipokuwa ameajiriwa na kujiajiri mwenyewe 
jambo hilo la kukurupuka kujiajiri ni baya sana kikubwa fahamu ata huyo boss wako kajiajiri ndipo akakuajiri wewe ukishagundua hilo tuliza akili pangilia mipango yako ya jinsi gani utaendesha biashara yako kwa kujiajiri wewe mwenyewe

HAYA NDIO MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUJIAJIRI

01. JENGA HESHIMA; najua wengi mtakuwa mnajiuliza nijengaje heshima hii ipo hivi unatakiwa uheshimu kwanza kile ambacho unachotaka kukifanya baada ya hapo heshimu muda wako .kama hauwezi kuuheshimu ata mda wako wa kazi daima utajutia tu kujiajiri kwasababu unapojiajiri amna mtu wa kukupelekesha kwamba mda huu fanya kitu fulani hapo ni wewe mwenyewe 
kwahiyo tunatakiwa kuheshimu muda wetu 
02. TAMBUA JAMII INATAKA NINI KWA WAKATI HUO;hili ni jambo kubwa sanaunapotaka kujiajiri hakikisha jamii inayokuzunguka inataka nini kwa mda huo 
yaani kwa upande mwingine changamoto ambayo ipo kwa wakati huo katika jamii yako hiyo ndio fursa kwako kuanzisha biashara ambayo itakuingizia pesa nyingi sana
03.JIUNGE NA WAJASIRIAMALI/WAFANYA BIASHARA WALIOKUTANGULIA;
pia hichi ni kitu kitakachokusaidia sana wewe unayetaka kujiajiri kama wote tunavojua kuwa kila biashara ina changamoto zake kwahiyo unapojichanganya na wajasiriamali/wafanya biashara waliokutangulia utafahamu changamoto utakazoenda kukutana nazo mbele lakini hiyo haitakuwa mbaya kwako kwasababu tayaari umepewa njia ambazo utazitumia kupambana na changamoto hizo kwa kujichanganya na wajasiliamali/wafanyabiashara
04. BIDII;kama wote tunavojua kuwa katika kujiajiri kunahitaji bidii sana kwasababu tuchukulie mfano kwamba wapo wafanyabiashara wa nguo watano katika eneo moja nawewe upo ndani ya hao
swali unaweza kufanikiwa pasipo kuongeza bidii kwa kupunguza nguo bei kidogo ili kuweza kuwavutia wateja kikubwa bidii bidii bidii
05.FURAHIA UNACHOKIFANYA;siku zote ukifurahia unachokifanya utafanya kitu bora kwasababu utafanya kwa moyo mmoja .kwahiyo wewe unayetaka kujiajiri na biashara uliyoichagua haufurahii kuifanya nakushauri ACHA BIASHARA HIYO kwasababu huko ni kupoteza muda na pesa zako mafanikio hutayapata kamwe kwasababu hutoifanya kwa mikono miwili
06.TAFUTA ENEO ZURI LA KUFANYIA BIASHARA;Hili ni la muhimu sana kwa sababu ukitafuta eneo zuri ambalo mfano kuna mkusanyiko wa watu lazima upate pesa kwasababu ya mkusanyiko huo wa watu

MUHIMU: utakapowekeza pesa nyingi ndipo utapata pesa nyingi zaidi pia ukafata mambo hayo kufanikiwa lazima
kama una maoni ushauri tuachie apo chini ili kwa umoja wetu tuyafikie mafanikio
IMEANDIKWA NA YUSUPH SWALEH

endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv

Jumatano, 18 Oktoba 2017

MTOTO WA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU(SOKOINE)AUWAWA

Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Tanzania marehemu Edward Moringe Sokoine, Kereto Sokoine ameauwa katika ugomvi ulitokea na mkewe hii leo jijini arusha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo, amethibitisha tukio hilo na kusema limetokea mchana huu, hivyo jeshi la polisi lipo eneo la tukio kufuatilia kwa undani kilichojiri mpaka kuuawa kwa Kereto sokoine.

KUTOKA MUUNGWANA
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv

Jumanne, 17 Oktoba 2017

TAKUKURU YAMPA ONYO KALI MH. JOSHUA NASSARI


Image result for MH JOSHUA NASSARI
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeita Waandishi leo Dar es salaam na kutoa onyo kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ambae alipeleka ushahidi wa rushwa kwa taasisi hiyo dhidi ya Mkuu wa Wilaya Arumeru Alexander Mnyeti.

TAKUKURU imesema “Ni kama Mh. Nassari na wenzie wanataka kulifanya hili swala kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria, namuonya Mh. Nassari ameshaleta taarifa yake kwetu, atuachie tufanye kwa mujibu wa sheria na sio kutushinikiza kama kauli aliyoitoa jana….. ‘nitaendelea kutoa series’ “

“Hii Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu tutachukua hatua za kisheria dhidi yake”

KUTOKA MUUNGWANA

Jumapili, 8 Oktoba 2017

BREAKING NEWS: WATOTO WANUSURIKA KIFO BAADA YA AJALI YA GARI YAO NA GARIMOSHI(TRENI)





Hiyo imetokea mda mfupi uliopitaa jijini tanga inasemekana chanzo inasemekana ni gari iliyokuwa imebeba watoto hao kuzima katikati ya reli
lakini watoto wamenusurika kwenye ajali hiyo baada ya kuruka kila mmoja kwa upande wake