This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
Jumamosi, 28 Oktoba 2017
Jumamosi, 21 Oktoba 2017
BARUA ZA KIMAPENZI ZA BARACK OBAMA HADHARANI
UKITAKA KUWA TAJIRI ACHA TABIA HIZI
Hichi ndicho kipaji kingine cha harmonize
kwa kipaji hicho unamshauri aendelee na music au aingie rasmi uwanjani
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal tv on youtube
Ijumaa, 20 Oktoba 2017
HIVI NDIVO KESI YA SCORPION INAVYOENDELEA
Alhamisi, 19 Oktoba 2017
ILI PENZI LIDUMU LINAHITAJI VITU HIVI
1. Imani
Upendo unahitaji imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasio onekana unatakiwa kuwa na imani na mwenzi wako imani katika mausiano ni muhimu sana kuaminiana toa wasiwasi kwa mwenzi wako mwamini kuwa amekuchagua wewe hakuna mwingine ukopeke yako.
2. Ujasiri
Upendo unahitaji uwe jasiri katika hali zote uajasiri katika kunena ujasiri kutenda, ujasiri katika kuuzungumzia upendo kwa mwenzi wako upendo unamhitaji mtu jasiri sio kitu rahisi kama wengine wanavyozungumzia.
3. Mawasiliano
Upendo unahitaji mawasiliano maana mawasiliano hutengeneza mahusiano bila mawasiliano huku na mahusiano ili ujenge msingi mzuri mzuri wa mahusiano yako unahitaji uwe mtu mzuri katika mawasiliano- mawasiliano yana uwezo mkubwa sana wa kutunza mahusiano hivyo upendo unahitaji mawasiliano.
4. Asante
Upendo unahitaji neno asante kwa mwenzi wako kwa lolote atakalo litenda kwako kama atakupa zawadi asante hasa kwa mpenzi wako ni neno muhimu sana na linaongeza nguvu ya mapendo uwe unatumia neno hili asante kwa mpenzi wako maana upendo unahitaji neno hili ASANTE. Hata baada ya kutoka katika tendo la ndoa sema asante maana ni tendo la ndoa ni matokeo ya mapendo. Hivyo upendo unahitaji ASANTE.
5. Haki
Upendo unahitaji haki unatakiwa umtendee haki mwenzi wako usimyime haki yake ya msingi kumtunza kumpenda na kumtimizia haki zake zote najua unajua haki za mapenzi wako- upendo ili ukomae unahitaji haki iwapo katika mahusiano yenu.
ENDELEA KUTUFUATILIA
Harmonize - Nishachoka (Official Video)
watch now nishachoka video by harmonize
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUJIAJIRI
najua watu wengi wanafikiria na wanahisi ni bora kujiajiri kuliko kuajiriwa hiyo ni sawa lakini wengi hukurupuka kuanza kujiajiri jambo ambalo mda mwingi linaleta madhara makubwa na mtu kuanza kujutia kwanini kaacha kazi alipokuwa ameajiriwa na kujiajiri mwenyewe
jambo hilo la kukurupuka kujiajiri ni baya sana kikubwa fahamu ata huyo boss wako kajiajiri ndipo akakuajiri wewe ukishagundua hilo tuliza akili pangilia mipango yako ya jinsi gani utaendesha biashara yako kwa kujiajiri wewe mwenyewe
HAYA NDIO MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUJIAJIRI
01. JENGA HESHIMA; najua wengi mtakuwa mnajiuliza nijengaje heshima hii ipo hivi unatakiwa uheshimu kwanza kile ambacho unachotaka kukifanya baada ya hapo heshimu muda wako .kama hauwezi kuuheshimu ata mda wako wa kazi daima utajutia tu kujiajiri kwasababu unapojiajiri amna mtu wa kukupelekesha kwamba mda huu fanya kitu fulani hapo ni wewe mwenyewe
kwahiyo tunatakiwa kuheshimu muda wetu
02. TAMBUA JAMII INATAKA NINI KWA WAKATI HUO;hili ni jambo kubwa sanaunapotaka kujiajiri hakikisha jamii inayokuzunguka inataka nini kwa mda huo
yaani kwa upande mwingine changamoto ambayo ipo kwa wakati huo katika jamii yako hiyo ndio fursa kwako kuanzisha biashara ambayo itakuingizia pesa nyingi sana
03.JIUNGE NA WAJASIRIAMALI/WAFANYA BIASHARA WALIOKUTANGULIA;
pia hichi ni kitu kitakachokusaidia sana wewe unayetaka kujiajiri kama wote tunavojua kuwa kila biashara ina changamoto zake kwahiyo unapojichanganya na wajasiriamali/wafanya biashara waliokutangulia utafahamu changamoto utakazoenda kukutana nazo mbele lakini hiyo haitakuwa mbaya kwako kwasababu tayaari umepewa njia ambazo utazitumia kupambana na changamoto hizo kwa kujichanganya na wajasiliamali/wafanyabiashara
04. BIDII;kama wote tunavojua kuwa katika kujiajiri kunahitaji bidii sana kwasababu tuchukulie mfano kwamba wapo wafanyabiashara wa nguo watano katika eneo moja nawewe upo ndani ya hao
swali unaweza kufanikiwa pasipo kuongeza bidii kwa kupunguza nguo bei kidogo ili kuweza kuwavutia wateja kikubwa bidii bidii bidii
05.FURAHIA UNACHOKIFANYA;siku zote ukifurahia unachokifanya utafanya kitu bora kwasababu utafanya kwa moyo mmoja .kwahiyo wewe unayetaka kujiajiri na biashara uliyoichagua haufurahii kuifanya nakushauri ACHA BIASHARA HIYO kwasababu huko ni kupoteza muda na pesa zako mafanikio hutayapata kamwe kwasababu hutoifanya kwa mikono miwili
06.TAFUTA ENEO ZURI LA KUFANYIA BIASHARA;Hili ni la muhimu sana kwa sababu ukitafuta eneo zuri ambalo mfano kuna mkusanyiko wa watu lazima upate pesa kwasababu ya mkusanyiko huo wa watu
MUHIMU: utakapowekeza pesa nyingi ndipo utapata pesa nyingi zaidi pia ukafata mambo hayo kufanikiwa lazima
kama una maoni ushauri tuachie apo chini ili kwa umoja wetu tuyafikie mafanikio
IMEANDIKWA NA YUSUPH SWALEH
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
HAYA HAPA MADHARA YA KUTOFANYA TENDO LA NDOA KWA MDA MREFU
- Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
- kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
- Kusahausahau,
- Kupendelea story za mapenzi,
- Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
- Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
- Kuumwa na kichwa,
- Kukakamaa mgongo (wanaume),
- Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
- Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
- Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
- Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala
Jumatano, 18 Oktoba 2017
EXCLUSIVE : Alichosema LULU baada ya kesi ya mauaji ya KANUMBA kuanza upya
Hiyo ni kutoka RICK MEDIA
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
JUX: KUMCHAGUA VANESSA MDEE AU MWANAMITINDO HUDDAH?
Hiyo ni baada ya Mwanamitindo na Mfanyabiashara kutoka Kenya, Huddah Monroe, amefunguka na kusema kwamba anadhani Msanii Juma Jux wa Tanzania ni mwanaume ambaye yeye anaweza kuwa naye kimahusiano huku akimmwagia sifa kuwa anamuonekano mzurii kwenye mavazi.
Akifanya mahojiano maalumu na mtangazaji mmoja wa kituo cha television. Huddah alijibu swali la mtangazaji huyo kama anaweza kuwa kwenye mahusiano na Jux baada ya kumsifia kuwa ana muonekano wa tofauti na wenye kuvutia.
"Aaah, Nafikiri ni mwanaume ambaye naweza kuwa naye kwenye mahusiano...... Yupo 'single? hata mimi nitapatikana....." amesema Huddah
Aidha Huddah amemshauri Jux kufanya kolabo na wasanii wakubwa zaidi wa kimataifa ili azidi kuwa msanii kubwa zaidi ndani na nje ya kimataifa kwani anamuonekano wa kuwa mtu maarufu.
Mbali na hayo Huddah amekiri kwamba alishawahi kumcheki Jux kupitia mtandao na kumwambia jinsi gani anapenda muonekano wake wa mavazi na jinsi ambavyo anavaa tofauti na jinsi jamii zinavyomfikiria.
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
SHULALA YA HARMONIZE YAUFUNGUA MOYO WA WOLPER TENA
hali iliyopelekea kila mmoja wao kuingia kwenye mapenzi na mtu mwingine tukianza kwa upande wa wolper yeye alijikuta ameingia katika mapenzi na kijana anayejulikana kama BROWN pia kwa upande wa harmonize kuingia kwenye mapenzi na mzungu anayejulikana kwa jina la SARA
lakini siku tatu nyuma baada ya harmonize kuachia brand new video inayokwenda kwa jina la SHULALA aliyomshirikisha koredebello
nyimbo hiyo imeonekana kumkuna sana wolper hali iliyompelekea kupost katika kurasa yake ya instagram hiyo post
- wolperstylishWe shulala wewe lala kesho sale @houseofstylish_tz #Darfremaket 61 msisahau kucheq shulala kwa bwana Raj @harmonize_tz
Kwa Bio yangu pia ukiingia utaona full vdio 👌 - hiyo ndiyo post aliyopost wolper na hiyo moja kwa moja inaonyesha kuwa wolper hana kinyongo chochote na harmonize
- tusubiri tuone kama penzi lao linaweza kurudi tena kama la vanessa na jux au harmonize atakubali kumuachia mzungu wake sarah
- endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
- pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
MTOTO WA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU(SOKOINE)AUWAWA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo, amethibitisha tukio hilo na kusema limetokea mchana huu, hivyo jeshi la polisi lipo eneo la tukio kufuatilia kwa undani kilichojiri mpaka kuuawa kwa Kereto sokoine.
KUTOKA MUUNGWANA
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
Jumanne, 17 Oktoba 2017
TAKUKURU YAMPA ONYO KALI MH. JOSHUA NASSARI
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeita Waandishi leo Dar es salaam na kutoa onyo kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ambae alipeleka ushahidi wa rushwa kwa taasisi hiyo dhidi ya Mkuu wa Wilaya Arumeru Alexander Mnyeti.
TAKUKURU imesema “Ni kama Mh. Nassari na wenzie wanataka kulifanya hili swala kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria, namuonya Mh. Nassari ameshaleta taarifa yake kwetu, atuachie tufanye kwa mujibu wa sheria na sio kutushinikiza kama kauli aliyoitoa jana….. ‘nitaendelea kutoa series’ “
“Hii Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu tutachukua hatua za kisheria dhidi yake”
KUTOKA MUUNGWANA
Jumatatu, 16 Oktoba 2017
MOURINHO ADHIBITISHA KUONDOKA UNITED.....!
Hapo mwanzoni kulikuwa na habari kwamba kocha Jose Mourinho angeongeza mkataba mpya utakaomuweka OT hadi mwaka 2022, lakini habari imebadilika na habari ni Jose Mourinho kuondoka United.
Mourinho ambaye amekuwa hana tabia ya kudumu katika klabu moja amesema ana uhakika hatamaliza kazi yake ya ukocha katika klabu hiyo na baada ya muda atakwenda kwingine, wapi anaweza kwenda hapo baadae?
Bayern Munich, kocha wa sasa wa Munich Jupp Heynckes mkataba wake na timu hiyo unaishi mwisho wa msimu huu, Mourinho anependa siku moja kupata mafanikio Ujerumani na hata kama sio msimu ujao inawezekana siku moja mbeleni Mou akatua Bayern Munich, mapenzi yake na vilabu vikubwa pia inaweza kumvuta Bayern.
Paris Saint German, amepata mafanikio Hispania, Italia, Uingereza na ni wazi angependa kwenda katika ligi nyingine yenye mvuto na inayokuja kwa kasi ulimwenguni, PSG ni mahala sahihi kwa Mourinho na patakuza sana jina la klabu.
Uingereza, kuna wakati nchini Uingereza Jose Mourinho alikuwa akipigiwa chapuo kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, japo hilo bado halijatokea lakini ni wazi baada ya mafanikio katika klabu Mou angependa kupata mafanikio timu ya taifa.
Ureno, ukiachana na Waingereza kumtaka lakini yeye Jose Mourinho amewahi kukiri kwamba kabla hajastaafu angependa kuifundisha nchi yake, kwa umri alionao hivi sasa inawezekana ndio muda sahihi wa kurudi nchini kwao kujiunga na timu ya taifa ya Ureno.
China League, Wachina nao huwezi kuwaacha kila mahala unapozungumzia jina kubwa, wanatumia nguvu kubwa ya pesa kujaribu kushawishi majina makubwa kuhamia katika vilabu vyao, na kama walivyowashawishi kina Carlos Tevez wanaweza kumshawishi pia Jose MourinhO
Jumatano, 11 Oktoba 2017
MFAHAMU KWA UFUPI TBWAY360 WA 5SELEKT
RAPA EMINEM AMTUKANA RAISI WA MAREKANI DONALD TRUMP
Rais wa Marekani, Donald Trump amekumbana na mistari 11 ya matusi kutoka kwa rapa, Eminem ambaye ametoa wimbo maalumu aliouita Came to Stomp.
Eminem alighani mistari hiyo ya dakika 4.5 katika utoaji wa tuzo za muziki za BET zilizotolewa jana Jumanne nchini Marekani.
Hii si mara ya kwanza kwa Eminem kumkosoa Trump isipokuwa amekuja kivingine. Wakati wa uchaguzi mwaka jana, Eminem alighani mashairi ya kuwatusi mashabiki wa Trump lakini sasa amekwenda hatua moja akimwita ‘Babu Mbaguzi’ na majina mengine ambayo ni matusi ya nguoni.
Katika moja ya mashairi yake anasema Trump ni mbaguzi na mchokozi ambaye anaweza kuanzisha vita ya nyuklia lakini akakimbilia juu na ndege yake mpaka mabomu yatakaposimama kurushwa.
“Ni askari ambaye ataanzisha vita lakini atajaza mafuta katika ndege na kukimbilia anga la juu akiwaacha watu wakifa,” anaghani Eminem.
Katika mstari mwingine anamtusi Trump kwa kupenda kushindana na watu wanaompinga kwa mabishano katika mtandao wa Twitter na kuwapuuza wananchi wanaoteseka baada ya maeno mbalimbali ya nchi hiyo kukumbwa na kimbunga
KUTOKA MUUNGWANA
ENDELEA KUTUFUATIA KUPITIA YUZHASSAL.BLOGSPOT.COM
PIA YOUTUBE KUPITIA YUZHASSAL TV
ANGALIA VIONJO VYA COLLABO YA DIAMOND PLATNUMZ FT RICK ROSE
Jumanne, 10 Oktoba 2017
MH RAILA ODINGA AJITOA KWENYE UCHAGUZI MKUU KENYA
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya anayejulikana kama Raila Odinga, ametangaza kuwa hatoshiriki kwenye uchaguzi mkuu wa kenya uliopagwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
mh Raila Odinga amesema anataka uchaguzi kufanyika mpya kama jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu
ya Uchaguzi huo uliofanyika tarehe 26 ambapo awali MH odinga alishindwa katika uchaguzi huo amesema odinga utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
FAHAMU MADHARA MAKUBWA YA KUVAA VIATU BILA SOKSI
Jumatatu, 9 Oktoba 2017
FARID KUBANDA(FID Q)ASEMA MATUSI NDIO YANAPELEKEA USTAR
Hayo farid kubanda amefunguka katika interview aliyofanya leo mida ya mchana na kituo kikubwa cha television
hayo alifunguka baada ya kuulizwa alichukuliaje matusi aliyoporomoshewa na watu tofautitofauti katika track yake iliyofanya vizuri sana inayokwenda kwa jina la FRESH REMIX aliyomshirikisha DIAMOND PLATNUMZ na RAYMOND wote kutoka katika kundi la WCB wasafi lakini akasema aliyachukulia poa matusi hayo kama njia ya kumtangaza zaidi
hilo ni funzo kwetu pia ukiona unapiga hatua halafu wanatokea watu wanaofikiria kukukatisha tamaa kwa matusi cheka tumia hayo matusi kama njia ya kusuccess
endelea kutufuatilia kwa kutumia yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv
NJIA KUMI ZA KUKUFANYA UWE SUMAKU INAYOVUTA PESA POPOTE PALE
Kwa kusoma tu hiko kichwa cha habari kwamba kuna namna unaweza kuwa sumaku ya fedha, kuna watu tayari wameshakuwa hasi, kwamba kwa nini huyu Makirita anaandika kuhusu fedha, kwanza yeye anazo kiasi gani, na mengine mengi. Nakuelewa kama wewe ni mmoja wa watu wenye hisia hizi hasi, kwa sababu halikuwa kosa lako kuwa nazo, ila kama utasoma hapa mpaka mwisho na ukaendelea kuwa na hisia hizo, hapo sasa ni kosa lako.
Tutakachokwenda kujifunza hapa ni kwamba wewe unaweza kuivuta fedha ije kwako, na kwa njia za kawaida kabisa, wala sio kwa nguvu ambazo hazieleweki kama wengi wanavyodanganyana. Zipo njia zilizodhibitishwa kisayansi ambazo zinafanya kazi kwa watu wote bila ya kujali kiwango cha elimu, rangi, au unatokea familia gani.
Nina hakika umewahi kusikia usemi kwamba mwenye nacho huongezewa, ya kwamba tajiri ataendelea kuwa tajiri na masikini ataendelea kuwa masikini. Huu ni usemi uliowekwa na watu walioliona hilo likiendelea kwa wengi, lakini wakashindwa kulichimba kwa undani. Ukweli ni kwamba tajiri anaendelea kuwa tajiri kwa sababu ameshakuwa sumaku ya fedha, anajua jinsi ya kuzivuta zije kwake. Na masikini anaendelea kuwa masikini kwa sababu hajaijua mbinu ya kuzivuta fedha zije kwake. Je unataka kuzijua mbinu za kuvutia fedha zije kwako?
Karibu tujifunze mambo haya kumi unayoweza kuanza kufanya leo kwenye maisha yako na ukazivutia fedha kuja kwako.
1. Kuwa mkarimu, wasaidie wengine kwa chochote unachofanya.
Njia ya kwanza kabisa ya kuzivutia fedha kuja kwako ni kuwa mkarimu. Chochote kile ambacho unakifanya kwenye maisha yako, iwe kazi au biashara, hakikisha lengo la kwanza ni kuwasaidia watu. Unawasaidia watu kwa kuwapa huduma ambazo ni bora na zinawaondolea maumivu wanayopata sasa au kuwapatia mahitaji wanayokosa sasa.
2. Kuwa na shukrani kwa fedha ulizonazo.
Haijalishi ni fedha kiasi gani unapata, hata kama ni kidogo sana, kitu muhimu kabisa ni kushukuru. Shukuru kwamba umepata nafasi ya kupata kiasi hiko cha fedha, ukijua ya kwamba kuna wengine wengi ambao hawajapata nafasi kama yako. Ukikutana na shilingi mia njiani wakati unapita, iokote kwa furaha.
Unapokuwa mtu wa shukrani unakaribisha zaidi kile ambacho unashukuru. Wengi huwa walalamikaji kwa fedha kidogo wanazopata na hapa wanafukuza zaidi nafasi yoyote ya kupata zaidi. Kuwa mtu wa shukrani, utavutia fedha nyingi zaidi.
3. Usiwaonee wivu wengine.
Kama kuna watu wengine wenye fedha nyingi kuliko wewe, usiwaonee wivu, badala yake wabariki. Mafanikio ya wengine siyo sababu ya wewe kushindwa. Na unapojenga wivu dhidi ya wengine unaiambia akili yako kwamba kuwa na fedha siyo kitu kizuri na hivyo inazikimbia fursa za fedha. Lakini unapowabariki wale wenye fedha kuliko wewe, unaifungua akili yako na kuziona fursa nyingi zaidi za kifedha.
4. Usijione mwenye hatia kwa kuwa una fedha nyingi.
Moja ya vitu vinavyowafanya wengi kutokuvutia fedha ni kujiona kama wakiwa na fedha nyingi basi wale wanaowazunguka hawatajisikia vizuri. Huku ni kujiona mwenye hatia kama utakuwa na fedha. Na kujiona mwenye hatia kutaiambia akili yako iepuke mazingira yoyote yanayoweza kukuletea fedha zaidi. Jione kuwa wa msaada kama utakuwa na fedha nyingi zaidi, na utazivutia zaidi na zaidi.
5. Kuwa na mapenzi makubwa kwenye kile unachofanya.
Chochote unachofanya kwenye maisha yako, jambo muhimu kabisa ni ukipende sana. Penda kile unachofanya. Kuna usemi unasema kama kazi yako ni kitu unachopenda, hutafanya kazi kwenye maisha yako. Na mwingine fanya kile unachopenda na fedha haitakuwa tatizo kwako. Fanya kitu unachopenda kufanya, iwe ni kazi au biashara, na weka moyo wako wote kwenye kitu hiko na hakuna kitu kinaweza kukuzuia wewe kupata fedha zaidi.
Wengi wamekuwa wakifanya vitu ambavyo hawavipendi ili tu wapate fedha, na wanashangaa kwa nini hawazipati, jibu ni kwa sababu wanazifukuza wao wenyewe. Unapofanya unachopenda, unazivutia fedha kuja kwako.
6. Ukipoteza fedha, usijione mnyonge na kulalamika.
Pale unapopoteza fedha, na lazima utapoteza iwe ni kwa hasara au kudhulumiwa, usianze kulalamika kwa nini inatokea kwako tu, bali jifunze ni nini kimepelekea wewe kufikia kwenye hali hiyo. Na hakikisha hurudii tena makosa ambayo uliyafanya awali na yakakufikisha hapo. Labda unahitaji kuwa makini zaidi, labda unahitaji kuangalia wale unaowaamini na mengine mengi.
Ukiishia tu kulalamika na kuona wewe huna hatia, utaendelea kurudia makosa yale yale na kamwe hutazivutia fedha kuja kwako.
7. Siku zote timiza ahadi zako.
Fanya kile ambacho umeahidi utafanya, na kikamilishe kwa wakati na kwa ubora. Usiwe mtu wa kuahidi kwa maneno na wakati wa matendo huonekani. Timiza ahadi zako na utavutia fedha nyingi zaidi kwako. Iwe ni kwenye kazi au kwenye biashara, unachomwahidi mwajiri wako kitimize, na hatakuwa na jinsi bali kukuthamini zaidi. Chochote unachomwahidi mteja wako timiza, na atapata huduma bora zitakazomfanya awe mteja wako wa kudumu na kuwaambia wengine wengi zaidi.
8. Tegemea kuwa tajiri.
Haijalishi maana yako ya utajiri ni nini, tegemea kuwa tajiri. Na usiishie tu kutegemea bali kuwa na mpango kabisa wa jinsi gani utafikia utajiri wako, kipato chako kiwe kiasi gani, uwekeze kiasi gani ili uweze kufikia utajiri. Utajiri hauji kama ajali, ni zao la malengo, mipango na juhudi kubwa. Kama hutegemei kuwa tajiri huwezi kuvutia fedha kwako.
9. Amini kwenye wingi.
Kuna fedha nyingi sana kwenye dunia hii, nyingi mno, japo wengi wanakushawishi kwamba kuna uhaba wa fedha, siyo kweli. Amini kwenye wingi wa fedha na unachohitaji ni wewe kuja na wazo zuri la kuwasaidia watu na watakuwa tayari kukupa fedha zaidi na zaidi. Dunia haina uhaba wa fedha na mali, bali ina uhaba wa mawazo mazuri ya kuboresha maisha, njoo na mawazo mazuri na utavutia fedha zaidi na zaidi.
10. Kuwa mkweli kwako, kuwa halisi.
Linapokuja swala la fedha na utajiri, watu wengi sana sio wa kweli kwao binafsi na hata kwa wengine. Watu wengi sio halisi, bali ni feki, wengi wanaigiza maisha ya utajiri na wakati hali zao sivyo zilivyo. Wengi wanakazana waonekane kwa nje wana utajiri kumbe ndani yao mambo ni magumu. Watu wanaingia kwenye madeni makubwa ili tu kuonekana nao wapo. Hii sio njia nzuri ya kuvutia fedha zije kwako, badala yake utazikimbiza zaidi. Njia bora ya kuvutia fedha kuja kwako ni kuwa mkweli, na kuwa halisi. Ishi yale maisha ambayo ni yako, usitake kuleta maigizo, hakuna yeyote unayemfaidisha na badala yake unajiumiza mwenyewe.
Hizo ndiyo njia kumi za kuzivutia fedha zije kwako na hatimaye uwe tajiri. Wote tunajua fedha ni muhimu, na kadiri unavyokuwa nazo nyingi inakuwa rahisi kwako kupata mahitaji ya msingi ya maisha yako, na hata kuwasaidia wengine pia.
Njia zote hizi kumi zinaanza na wewe binafsi, haiangalii elimu yako ni kiasi gani, rangi ya ngozi yako, au kabila unalotokea. Pia haziangalii umri wako au umetoka familia ya aina gani. Ni wewe ufanye maamuzi leo na uanze kutekeleza hayo. Na ujue inachukua muda, siyo jambo la kutokea mara moja, hivyo kuwa mvumulivu.
Neno la mwisho kabisa ninalotaka kukushirikisha ni kukuambia uchukue hatua, iwe utayafanyia haya kazi, au utayakataa na kuendelea na maisha yako ya sasa. Maamuzi ni yako wewe mwenyewe. Lakini jua hakuna mtu atakayekuja kukutoa hapo ulipo, utajitoa wewe mwenyewe.
NJIA KUU KUMI ZA KUMRUDISHA EX WAKO(BOYFRIEND/GIRLFRIEND)
Kuachana na mpenzi wako ni kitu cha kawaida watu hupitia kila siku. Aidha inawezakuwa mmeachana kwa sababu ya kukosana, kutoaminiana, kusalitiana na sababu nyingine nyingi ambazo unazijua wewe.
Aidha, unaweza kukosana na mpenzi wako kwa kosa dogo sana mpaka ukawa unajiuliza maswali ni kwa nini ama ni kitu gani kilichofanya ukosane na mpenzi wako. Wengine inafikia mahali wanatamani kurudiana na wapenzi wao.
Enyewe inaweza kuwa ngumu unapoachana na mpenzi wako haswa ukizingatia yale mambo yote mazuri ambayo mumekuwa mkifanya mkiwa pamoja. Vile vicheko, tabasamu, saprizes, nk inasisimua.
So utafanyaje urudiane na ex wako? Mbinu zenyewe za kufuata ndizo hizi:
#1 Mtumie Ex wako SMS. Kila kitu huanza na hatua ya kwanza. Mtumie ujumbe wa kawaida tu. Si lazima uandike jumbe ndefu ambayo inaweza kumuuliza kichwa. Unaweza kumtumia jumbe ‘Habari za masiku’. Hapa anaweza kukujibu kinjia mbili. Anaweza kuwa na jibu chanya au hasi. Jibu chanya ni majibu ambayo ni kuonyesha ameridhika kwa kumjulia hali. Anaweza kujibu, ‘Asante kwa kunijulia hali, unaendeleaje?’. Hakikisha humtumii jumbe wakati wote. Jumbe mbili-tatu zinatosha kwa siku. Mwache yeye aanze aproach.
#2 Nenda polepole bila pupa. Kurudiana na Ex wako kunahitaji hatua ya polepole. Hii ni kumaanisha usiingize hisia za mapenzi kwayo. Unataka urudiane na Ex wako hivyo lazima uende na spidi yake. Usiende mbio wakati breki anaikontroli yeye. Pia iheshimu himaya binafsi yake. Ukiwa unaongea naye ana kwa ana weka nafasi kati yako na yeye.
#3 Mpigie simu mara kwa mara. Mpigie simu mara kwa mara. Lakini kama nilivyotangulia kusema katika hatua ya kwanza usiwe na pupa. Usimpigie kila lisaa. Anza kwa kumpigia mara moja kwa siku/mbili. Halafu punguza huo muda pole pole mpaka iwe mazoea ya kumpigia simu. Hii itakuwa na mpigo mkuu kufufua hisia zenu.
#4 Mwambie kuwa unammiss. Mwambie unammisi. Yafanye mazungumzo yenu yawe sahili mwanzo mwanzo. Usimpresha na mambo mazito. Usimkumbushe mambo ambayo yalichangia kwenu kuachana. Tayari anajua. So wewe makinika na kumwonyesha kuwa unamisi uwepo wake kwako. Hakikisha hukumbushi matukio yaliyochangia kuachana kwenu.
#5 Fanya yale mambo madogo madogo. Kufanya mambo madogo madogo kunachangia kuleta mabadiliko. Kwa mfano akitaka usaidizi mdogo wewe unajitokeza unamsaidia bila kuitisha chochote.
#6 Makinika na hisia chanya zenu za awali. Zungumza yale mambo mazuri mliokuwa mnapitia pamoja. Mambo ambayo yaliwafanya mkawa kitu kimoja. Hakikisha kuwa unaepuka kuzungumza mambo yeyote mabaya. Hisia chanya kutachangia kufufua chembechembe zozote za mapenzi ambazo alikuwa nazo.
#7 Tangamana na marafiki wenu wa awali. Kama ameamua kutoka out, hakikisha unatoka na marafiki wenu wa awali. Hakikisha hauzui hisia zozote. Tembea na yeye bila kuwa na hisia zozote. Mchukulie kama rafiki yako tu.
#8 Usizungumzie maisha yako baada ya kuachana. Usijaribu kuyafananisha maisha yako ya sasa na yale ya awali. Usiongee kuhusu maisha yamekuwa magumu ama mazuri tangu uachane na yeye la sivyo utaongeza chumvi ndani ya kidonda.
#9 Usimuombe. Kosa ambalo wengi hufanya ni kumpigia Ex wake magoti na kumwomba warudiane. Ukifanya hivi utakuwa unampa ishara ya kuwa wewe huwezi kujitegemea kivyako hivyo kumfanya akutenge zaidi. Unachotakiwa kufanya ni kuonyesha confidence.
#10. Enjoy romance. Baada ya kuwasiliana, kumweleza hisia zako na kuingiliana, sasa hapa una nafasi ya kuendeleza romance kama kawaida. Ukifuata mbinu tulizoziorodhesha awali vizuri basi kila kitu kitakuja natural.
Ok. Hizi ndizo mbinu za kufuata kumrudisha Ex wako. Lakini kabla kuchukua hatua hii unapaswa kwaza kujiuliza ni kitu gani kilichochangia nyinyi wawili kuachana. Na je, ukirudiana naye hamtakosana tena