Mwanamuziki wa bongo fleva na dancer msami ameweza kufunguka mambo mengi sana alipofanya mahojiano na @shadee_weriss wa clouds E ya clouds tv
Kwanza kabisa ni pale alipooulizwa kuhusiana na colabo yake bora ya mwaka 2017 na akaitaja collabo aliyofanya na chemical
Jambo la pili ni pale alipoulizwa kwamba ni yupi msanii bora kwake kwa mwaka 2017
Msami kwa hisia kali aliweza kufunguka kwamba msanii bora kwake 2017 ni aslay
Jambo la mwisho lililotaka kumtoa machozi msami ni pale alipoulizwa "kitu ambacho hawezi kukisahau kwa mwaka 2017"
Msami alifunguka kwa hisia Kali na kusema ni pale alipopata ajali iliyoyompelekea kushindwa kufanya baadhi ya shows na zingine alizojikaza kisabuni kuzifanya hazikuwa katika quality ya msami
Lakini msami hakusita kutoa shukrani kwa watu waliokuwa nae bega kwa bega katika matatizo hayo kwa kumtaja kwanza kabisa manager wake,wazazi wake lakini pia marafiki zake wa karibu
Imeandikwa na yusuph swaleh
0 comments :
Chapisha Maoni