FOR THE ENTERTAINMENT UPDATES & INTERVIEWS

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Jumatano, 11 Oktoba 2017

MFAHAMU KWA UFUPI TBWAY360 WA 5SELEKT



Jina lake halisi alilopewa na wazazi wake ni Tony Albert.
Alizaliwa Tarehe 10/06 jijini Mwanza na kukulia ndani ya jiji la Dar es Salaam.
katika upande wa elimu TBWAY360 alisoma shule za Esaacs Primary School na Kampala International High School.
tony albert maarufu kama Tbway360 ana urefu wa futi 6.5
vitu anavyovipenda mtangazaji huyo ni kupiga picha, kuogelea, movie kusikiliza music na kuendesha magari kwa kasi zaidi.
najua watu wengi mtakuwa na hamu ya kufahamu ilikuwaje mpaka akapachikwa jina la TBWAY360 jibu ni hili apa  Alipachikwa jina la TBWAY 360 akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kuzungusha gari mzunguko wa duara yaani nyuzi 360
leo kwenye STATUS nilikuwa na TBWAY360
kesho unafahamu nipo na nani___________________________endelea kutufuatilia ili kujua nipo na nani katika STATUS ya YUZHASSAL TV

RAPA EMINEM AMTUKANA RAISI WA MAREKANI DONALD TRUMP

                 


Rais wa Marekani, Donald Trump amekumbana na mistari 11 ya matusi kutoka kwa rapa, Eminem ambaye ametoa wimbo maalumu aliouita Came to Stomp.

Eminem alighani mistari hiyo ya dakika 4.5 katika utoaji wa tuzo za muziki za BET zilizotolewa jana Jumanne nchini Marekani.

Hii si mara ya kwanza kwa Eminem kumkosoa Trump isipokuwa amekuja kivingine. Wakati wa uchaguzi mwaka jana, Eminem alighani mashairi ya kuwatusi mashabiki wa Trump lakini sasa amekwenda hatua moja akimwita ‘Babu Mbaguzi’ na majina mengine ambayo ni matusi ya nguoni.

Katika moja ya mashairi yake anasema Trump ni mbaguzi na mchokozi ambaye anaweza kuanzisha vita ya nyuklia lakini akakimbilia juu na ndege yake mpaka mabomu yatakaposimama kurushwa.

“Ni askari ambaye ataanzisha vita lakini atajaza mafuta katika ndege na kukimbilia anga la juu akiwaacha watu wakifa,” anaghani Eminem.

Katika mstari mwingine anamtusi Trump kwa kupenda kushindana na watu wanaompinga kwa mabishano katika mtandao wa Twitter na kuwapuuza wananchi wanaoteseka baada ya maeno mbalimbali ya nchi hiyo kukumbwa na kimbunga

KUTOKA MUUNGWANA
ENDELEA KUTUFUATIA KUPITIA YUZHASSAL.BLOGSPOT.COM
PIA YOUTUBE KUPITIA YUZHASSAL TV

ANGALIA VIONJO VYA COLLABO YA DIAMOND PLATNUMZ FT RICK ROSE











Hizo ni picha zilizotoka katika clip ndogo iliyoachiwa kwenye mtandao wa istagram na boss wake diamond platnumz anayejulikana kama salaam sk 
lakini meneja huyo ameamua kuificha kidogo ili kuwaongezea hamu mashabiki wa WCB wasafi baada ya kupost clip hiyo ya video na kuiweka mute yani kutokuwa na sauti 
jambo hilo limezidisha hamu kwa mashabiki wengi sana ulimwenguni 
pia collabo hiyo itakuwa na faida kwa nchi pia kwa diamond WCB kwaujumla kwasababu tukirejea miaka kadhaa nyuma ambapo CHRIS BROWN  alimtolea nje diamond platnumz ombi la kufanya collabo lakini kwa collabo hii itakayotoka soon kati ya diamond platnumz na rick rose inaweza kuwa chachu ya kumshawishi CHRIS BROWN kufanya collabo na DIAMOND PLATNUMZ 
Pia kwa upande wa faida kwa taifa kwasababu itakuwa chachu ya kuitangaza nchi yetu katika mataifa yaliyoendelea hiyo itakuwa rahisi kwa kutengenezwa collabo nyingine kati ya msanii mkubwa wa nje na msanii mwingine kutoka tanzania kwasababu watatambua kuwa  tanzania kuna vipaji vingi na vikubwa
endelea kutufuatilia kwa kuandika yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv

Jumanne, 10 Oktoba 2017

MH RAILA ODINGA AJITOA KWENYE UCHAGUZI MKUU KENYA



Image result for odinga
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya anayejulikana kama Raila Odinga, ametangaza kuwa hatoshiriki kwenye uchaguzi mkuu wa kenya uliopagwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

mh Raila  Odinga amesema anataka uchaguzi kufanyika  mpya kama  jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu
ya Uchaguzi huo uliofanyika  tarehe 26 ambapo awali MH odinga alishindwa katika uchaguzi huo amesema odinga utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu
.

FAHAMU MADHARA MAKUBWA YA KUVAA VIATU BILA SOKSI

Image result for KUVAA VIATU BILA SOKSI
Ukivalia viatu vyako bila soksi unajiweka katika hatari ya makubwa zaidi kuliko kunuka kwa miguu pekee.

Chuo cha tiba ya miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu kutokana na kuvuma kwa mtindo wa kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.

Mtaalamu Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia viatu visivyowatosha vyema.

Kutovalia soksi siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.

Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.

Mwanamuziki Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi katika maonesho ya mitindo ya Londo huketi viti vya mbele.

Yeye pia huwa mara nyingi havai soksi - lakini anafahamu madhara yake?

"Miguu ya binadamu kwa kawaida hutoa nusu painti (ambayo ni sawa na lita 0.28) ya jasho kila siku," Emma Stephenson anasema.

"Unyevu mwingi na joto unaweza kusababisha maambukizi ya maradhi yanayotokana na kuvu mfano ugonjwa unaosababisha mwasho na kuchubuka kwa ngozi (kwa Kiingereza athlete's foot)."

Kwa mujibu wa Emma, madhara yake yanaweza kuwa mabaya.

"Moja ya visa vibaya nilivyowahi kukumbana navyo ni cha mwanamume mmoja wa miaka 19 aliyefanya kazi ya kuosha magari. Miguu yake ilikuwa inatokwa na jasho sana na ilikuwa imechubuka sana."

Emma anashauri kwamba siri ni kutozidisha, iwapo bado utataka kutovalia soksi.

Jaribu usivae viatu bila soksi kwa muda mrefu.

Jaribu pia kuweka kitu cha kukausha jasho kwenye soli ya kiatu chako kabla ya kukivalia bila soksi.
Kadhalika, kuwa makini kuchunguza miguu yako.

KUTOKA MUUNGWANA 

Jumatatu, 9 Oktoba 2017

FARID KUBANDA(FID Q)ASEMA MATUSI NDIO YANAPELEKEA USTAR

Image result for FID Q
Hayo farid kubanda amefunguka katika interview aliyofanya leo mida ya mchana  na kituo kikubwa cha television
hayo alifunguka baada ya kuulizwa alichukuliaje matusi aliyoporomoshewa na watu tofautitofauti katika track yake iliyofanya vizuri sana inayokwenda kwa jina la FRESH REMIX aliyomshirikisha DIAMOND PLATNUMZ na RAYMOND wote kutoka katika kundi la WCB wasafi lakini akasema aliyachukulia poa matusi hayo kama njia ya kumtangaza zaidi
hilo ni funzo kwetu pia ukiona unapiga hatua halafu wanatokea watu wanaofikiria kukukatisha tamaa kwa matusi cheka tumia hayo matusi kama njia ya kusuccess
endelea kutufuatilia kwa kutumia yuzhassal.blogspot.com
pia youtube kwa kuandika yuzhassal tv

NJIA KUMI ZA KUKUFANYA UWE SUMAKU INAYOVUTA PESA POPOTE PALE

Image result for A MAN MAGNET FOR MONEY
Linapokuja swala la fedha, kila mtu ana hisia tofauti, na hisia hizi zinatokana na malezi ambayo tumepata kwenye jamii ambazo tumekulia. Na katika hisia hizi, nyingi huwa ni hasi, kwamba fedha ni kitu kibaya au kitu ambacho hakihitaji kujadiliwa mara kwa mara.

Kwa kusoma tu hiko kichwa cha habari kwamba kuna namna unaweza kuwa sumaku ya fedha, kuna watu tayari wameshakuwa hasi, kwamba kwa nini huyu Makirita anaandika kuhusu fedha, kwanza yeye anazo kiasi gani, na mengine mengi. Nakuelewa kama wewe ni mmoja wa watu wenye hisia hizi hasi, kwa sababu halikuwa kosa lako kuwa nazo, ila kama utasoma hapa mpaka mwisho na ukaendelea kuwa na hisia hizo, hapo sasa ni kosa lako.

Tutakachokwenda kujifunza hapa ni kwamba wewe unaweza kuivuta fedha ije kwako, na kwa njia za kawaida kabisa, wala sio kwa nguvu ambazo hazieleweki kama wengi wanavyodanganyana. Zipo njia zilizodhibitishwa kisayansi ambazo zinafanya kazi kwa watu wote bila ya kujali kiwango cha elimu, rangi, au unatokea familia gani.

Nina hakika umewahi kusikia usemi kwamba mwenye nacho huongezewa, ya kwamba tajiri ataendelea kuwa tajiri na masikini ataendelea kuwa masikini. Huu ni usemi uliowekwa na watu walioliona hilo likiendelea kwa wengi, lakini wakashindwa kulichimba kwa undani. Ukweli ni kwamba tajiri anaendelea kuwa tajiri kwa sababu ameshakuwa sumaku ya fedha, anajua jinsi ya kuzivuta zije kwake. Na masikini anaendelea kuwa masikini kwa sababu hajaijua mbinu ya kuzivuta fedha zije kwake. Je unataka kuzijua mbinu za kuvutia fedha zije kwako?

Karibu tujifunze mambo haya kumi unayoweza kuanza kufanya leo kwenye maisha yako na ukazivutia fedha kuja kwako.

1. Kuwa mkarimu, wasaidie wengine kwa chochote unachofanya.
Njia ya kwanza kabisa ya kuzivutia fedha kuja kwako ni kuwa mkarimu. Chochote kile ambacho unakifanya kwenye maisha yako, iwe kazi au biashara, hakikisha lengo la kwanza ni kuwasaidia watu. Unawasaidia watu kwa kuwapa huduma ambazo ni bora na zinawaondolea maumivu wanayopata sasa au kuwapatia mahitaji wanayokosa sasa.

2. Kuwa na shukrani kwa fedha ulizonazo.
Haijalishi ni fedha kiasi gani unapata, hata kama ni kidogo sana, kitu muhimu kabisa ni kushukuru. Shukuru kwamba umepata nafasi ya kupata kiasi hiko cha fedha, ukijua ya kwamba kuna wengine wengi ambao hawajapata nafasi kama yako. Ukikutana na shilingi mia njiani wakati unapita, iokote kwa furaha.

Unapokuwa mtu wa shukrani unakaribisha zaidi kile ambacho unashukuru. Wengi huwa walalamikaji kwa fedha kidogo wanazopata na hapa wanafukuza zaidi nafasi yoyote ya kupata zaidi. Kuwa mtu wa shukrani, utavutia fedha nyingi zaidi.

3. Usiwaonee wivu wengine.
Kama kuna watu wengine wenye fedha nyingi kuliko wewe, usiwaonee wivu, badala yake wabariki. Mafanikio ya wengine siyo sababu ya wewe kushindwa. Na unapojenga wivu dhidi ya wengine unaiambia akili yako kwamba kuwa na fedha siyo kitu kizuri na hivyo inazikimbia fursa za fedha. Lakini unapowabariki wale wenye fedha kuliko wewe, unaifungua akili yako na kuziona fursa nyingi zaidi za kifedha.

4. Usijione mwenye hatia kwa kuwa una fedha nyingi.
Moja ya vitu vinavyowafanya wengi kutokuvutia fedha ni kujiona kama wakiwa na fedha nyingi basi wale wanaowazunguka hawatajisikia vizuri. Huku ni kujiona mwenye hatia kama utakuwa na fedha. Na kujiona mwenye hatia kutaiambia akili yako iepuke mazingira yoyote yanayoweza kukuletea fedha zaidi. Jione kuwa wa msaada kama utakuwa na fedha nyingi zaidi, na utazivutia zaidi na zaidi.

5. Kuwa na mapenzi makubwa kwenye kile unachofanya.
Chochote unachofanya kwenye maisha yako, jambo muhimu kabisa ni ukipende sana. Penda kile unachofanya. Kuna usemi unasema kama kazi yako ni kitu unachopenda, hutafanya kazi kwenye maisha yako. Na mwingine fanya kile unachopenda na fedha haitakuwa tatizo kwako. Fanya kitu unachopenda kufanya, iwe ni kazi au biashara, na weka moyo wako wote kwenye kitu hiko na hakuna kitu kinaweza kukuzuia wewe kupata fedha zaidi.
Wengi wamekuwa wakifanya vitu ambavyo hawavipendi ili tu wapate fedha, na wanashangaa kwa nini hawazipati, jibu ni kwa sababu wanazifukuza wao wenyewe. Unapofanya unachopenda, unazivutia fedha kuja kwako.

6. Ukipoteza fedha, usijione mnyonge na kulalamika.
Pale unapopoteza fedha, na lazima utapoteza iwe ni kwa hasara au kudhulumiwa, usianze kulalamika kwa nini inatokea kwako tu, bali jifunze ni nini kimepelekea wewe kufikia kwenye hali hiyo. Na hakikisha hurudii tena makosa ambayo uliyafanya awali na yakakufikisha hapo. Labda unahitaji kuwa makini zaidi, labda unahitaji kuangalia wale unaowaamini na mengine mengi.
Ukiishia tu kulalamika na kuona wewe huna hatia, utaendelea kurudia makosa yale yale na kamwe hutazivutia fedha kuja kwako.

7. Siku zote timiza ahadi zako.
Fanya kile ambacho umeahidi utafanya, na kikamilishe kwa wakati na kwa ubora. Usiwe mtu wa kuahidi kwa maneno na wakati wa matendo huonekani. Timiza ahadi zako na utavutia fedha nyingi zaidi kwako. Iwe ni kwenye kazi au kwenye biashara, unachomwahidi mwajiri wako kitimize, na hatakuwa na jinsi bali kukuthamini zaidi. Chochote unachomwahidi mteja wako timiza, na atapata huduma bora zitakazomfanya awe mteja wako wa kudumu na kuwaambia wengine wengi zaidi.

8. Tegemea kuwa tajiri.
Haijalishi maana yako ya utajiri ni nini, tegemea kuwa tajiri. Na usiishie tu kutegemea bali kuwa na mpango kabisa wa jinsi gani utafikia utajiri wako, kipato chako kiwe kiasi gani, uwekeze kiasi gani ili uweze kufikia utajiri. Utajiri hauji kama ajali, ni zao la malengo, mipango na juhudi kubwa. Kama hutegemei kuwa tajiri huwezi kuvutia fedha kwako.

9. Amini kwenye wingi.
Kuna fedha nyingi sana kwenye dunia hii, nyingi mno, japo wengi wanakushawishi kwamba kuna uhaba wa fedha, siyo kweli. Amini kwenye wingi wa fedha na unachohitaji ni wewe kuja na wazo zuri la kuwasaidia watu na watakuwa tayari kukupa fedha zaidi na zaidi. Dunia haina uhaba wa fedha na mali, bali ina uhaba wa mawazo mazuri ya kuboresha maisha, njoo na mawazo mazuri na utavutia fedha zaidi na zaidi.

10. Kuwa mkweli kwako, kuwa halisi.
Linapokuja swala la fedha na utajiri, watu wengi sana sio wa kweli kwao binafsi na hata kwa wengine. Watu wengi sio halisi, bali ni feki, wengi wanaigiza maisha ya utajiri na wakati hali zao sivyo zilivyo. Wengi wanakazana waonekane kwa nje wana utajiri kumbe ndani yao mambo ni magumu. Watu wanaingia kwenye madeni makubwa ili tu kuonekana nao wapo. Hii sio njia nzuri ya kuvutia fedha zije kwako, badala yake utazikimbiza zaidi. Njia bora ya kuvutia fedha kuja kwako ni kuwa mkweli, na kuwa halisi. Ishi yale maisha ambayo ni yako, usitake kuleta maigizo, hakuna yeyote unayemfaidisha na badala yake unajiumiza mwenyewe.

Hizo ndiyo njia kumi za kuzivutia fedha zije kwako na hatimaye uwe tajiri. Wote tunajua fedha ni muhimu, na kadiri unavyokuwa nazo nyingi inakuwa rahisi kwako kupata mahitaji ya msingi ya maisha yako, na hata kuwasaidia wengine pia.

Njia zote hizi kumi zinaanza na wewe binafsi, haiangalii elimu yako ni kiasi gani, rangi ya ngozi yako, au kabila unalotokea. Pia haziangalii umri wako au umetoka familia ya aina gani. Ni wewe ufanye maamuzi leo na uanze kutekeleza hayo. Na ujue inachukua muda, siyo jambo la kutokea mara moja, hivyo kuwa mvumulivu.

Neno la mwisho kabisa ninalotaka kukushirikisha ni kukuambia uchukue hatua, iwe utayafanyia haya kazi, au utayakataa na kuendelea na maisha yako ya sasa. Maamuzi ni yako wewe mwenyewe. Lakini jua hakuna mtu atakayekuja kukutoa hapo ulipo, utajitoa wewe mwenyewe.